Wanawake wa JKCI washirikiana katika matukio ya kijamii

Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha wanawake JKCI Dkt. Angela Muhozya wakimkaribisha Afisa Muuguzi mstaafu wa Taasisi hiyo Rehema Bakari wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.


Afisa Muuguzi Mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rehema Bakari akikata keki wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanywa na wanawake wa Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa chama cha wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Angela Muhozya akimkabidhi zawadi ya kitenge Afisa Muuguzi mstaafu wa JKCI Rehema Bakari wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Chama hicho pia kimempatia Bi. Rehema zawadi ya fedha taslim Tshs. 1,300,000.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akimpa kitenge cha pole ya kuondokewa na mzazi wake mfanyakazi wa JKCI Eng. Veronica Mugendi wakati wa kikao cha wanawake wa JKCI kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. 


Mkuu wa Kitengo cha Dawa (Pharmacy) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wellu Kaali akimpa kitenge cha pole ya kuondokewa na mtoto wake Mhudumu wa Afya wa Taasisi hiyo Mereciana Michael wakati wa kikao cha wanawake wa JKCI kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI

****************************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)