Matibabu ya kibingwa ya moyo yatolewa Sabasaba
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanaotoa huduma katika banda la taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
Daktari wa huduma za dharura kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Nicole Kinyawa akiwafundisha wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo namna ya kumsaidia mgonjwa anayehitaji huduma ya dharura wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago akimuonyesha mwananchi aliyepata huduma katika banda la taasisi hiyo majibu ya kipimo cha shinikizo la damu wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikiwete (JKCI) Renata Kulwa akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa
umeme wa moyo mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho
ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildagard Karau akimwelezea huduma zinazopatikana katika banda la taasisi hiyo raia wa China alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akiwasajiri wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Picha na: Hamis Mussa
*******************************************************************************************************
Comments
Post a Comment