Posts

Showing posts from December, 2024

Wasanii waishukuru Serikali upimaji moyo Kawe

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Flora Zacharia akimpima Shinikizo la damu, mapigo ya moyo na kiwango cha oksijeni mwilini msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuhura Othman Soud (Zuchu) alipofika katika Kliniki ya Taasisi hiyo iliyopo Kawe kwaajili ya ufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuhura Othman Soud (Zuchu) mara baada ya kufanya vipimo vya moyo katika Kliniki ya Taasisi hiyo iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia majibu yake msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi Mbwana Yusuph Kilungi (Mbosso) mara baada ya kufanya vipimo vya moyo katika Kliniki ya Taasisi hiyo iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi D Voice Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)...

JKCI yafungua Kliniki Oysterbay

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na mwananchi aliyefika JKCI Kliniki ya Oysterbay iliyopo Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo wakati kliniki hiyo ilivyoanza kutoa huduma. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anord Mushi akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyefika JKCI Kliniki ya Oysterbay iliyopo Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo wakati kliniki hiyo ilivyoanza kutoa huduma. Mtunza kumbukumbu za afya (DPO) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mercy Msuya akimpa maelekezo mwananchi aliyefika JKCI Kliniki ya Oysterbay iliyopo Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo wakati kliniki hiyo ilivyoanza kutoa huduma. Mteknolojia wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Margareth Mtaita akimtoa damu kwaajili ya vipimo mwananchi aliyefika JKCI Kliniki ya Oysterbay iliyopo Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo wakati klinik...

Wasanii wapima moyo

Image

Wasanii watakiwa kuelimisha jamii kujikinga na magonjwa ya moyo.

Image
Baadhi ya wasanii wa bongo movie wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kawe iliyopo jengo la Mkapa Health Plaza jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akisikiliza mapigo ya moyo ya msanii wa bongo movie na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengele wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayofanywa na Taasisi hiyo kwaajili ya kuwafanyia uchunguzi na matibabu ya moyo wasanii katika Kliniki ya JKCI iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health jijini Dar es Salaam. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Devotha Mapunda akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) msanii aliyefika katika Kliniki ya JKCI iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya tiba mkoba ya...

Wafanyakazi wa JKCI wapewa zawadi za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimkabidhi Afisa Muuguzi Msaidizi wa Taasisi hiyo Veronica Mmari zawadi ya mafuta ya kupikia ikiwa ni moja ya zawadi   za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya zilizotolewa na uongozi wa Taasisi hiyo. Jumla ya wafanyakazi 719   wamepewa zawadi za sukari, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni   na unga wa ngano. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimkabidhi Afisa Kumbukumbu Msaidizi wa Taasisi hiyo Yusta Condra zawadi ya sukari ikiwa ni moja ya zawadi za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya zilizotolewa na uongozi wa Taasisi hiyo. Jumla ya wafanyakazi 719 wamepewa zawadi za sukari, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni   na unga wa ngano.  Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group    Dkt. Tulizo Shemu akimkabidhi Daktari wa taasisi hiyo Amisa Kaganda zawadi ya sukari ikiwa ni moja ya zawadi za sikukuu za Krismasi ...

Dawa za Shilingi 16,196,119 zatolewa bila malipo kwa wananchi wa Handeni

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Eva Wakuganda akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mtoto wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni iliyopo Wilaya ya Handeni vijijini mkoani Tanga. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Daniel Mkuyu akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiograph – ECG) mkazi wa Mkata wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni iliyopo Wilaya ya Handeni vijijini mkoani Tanga. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Eliza Shuma akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocard...

JKCI mshindi wa pili kundi la Hospitali kwenye usimamizi bora wa Rasilimaliwatu

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sanga akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha  Rasilimaliwatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdulrahman Muya tuzo ya Taasisi hiyo kwa kushika nafasi ya pili katika kundi la Hospitali kwenye usimamizi bora wa rasilimaliwatu iliyotolewa jana wakati wa mkutano mkuu wa wakurugenzi na wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu unaofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Selemani Mkomi. *************************************************************************************************************************************************************************************************************************** Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepata tuzo ya mshindi wa pili kundi la hospitali  kwenye  usimamizi bora wa rasilimali watu.   Tuzo hiyo imetolewa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawal...

411 wapimwa moyo Halmashauri ya Handeni Mjini

Image
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Handeni Dkt. Laurence Meshilieki akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika hospitali hiyo iliyopo mkoani Tanga. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mlagwa Yango akimpatia dawa mwananchi wa Handeni aliyepata huduma za uchuguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni iliyopo mkoani Tanga. Kushoto ni daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Handeni Antony Mwale Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima wingi wa sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba m...

DC Handeni aishukuru JKCI kwa kugusa mioyo ya wananchi

Image
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albart Msando akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo leo wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyika kwa siku mbili katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni iliyopo mkoani Tanga. Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albart Msando akipima shinikizo la damu leo baada ya ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyika kwa siku mbili katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni iliyopo mkoani Tanga. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akielezea namna taasisi hiyo imejipanga kuwafikia wananchi wote leo wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika kwa siku mbili katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni iliyopo mkoani Tanga.  Mkur...

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

Image
Mwenyekiti wa Chama cha kuweka akiba na mikopo (SACCOS) cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shem akizungumza na wanachama wa SACCOS hiyo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa Chama cha kuweka akiba na mikopo (SACCOS) cha JKCI akiwapongeza wanachama hao kwa kuweka jitihada za kuboresha mfuko wa SACCOS leo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam Afisa Ushirika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mihayo Malunde akielezea namna fedha zinazokusanywa na Chama cha kuweka akiba na mikopo (SACCOS) cha JKCI zinaweza kuongeza uchumi wa wanachama wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa SACCOS ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) uliofanyika leo katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam Mjumbe wa Chama cha kuweka akiba na mikop...