Naibu Waziri Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sanga
akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Abdulrahman Muya tuzo ya Taasisi hiyo kwa kushika nafasi ya pili
katika kundi la Hospitali kwenye usimamizi bora wa rasilimaliwatu iliyotolewa
jana wakati wa mkutano mkuu wa wakurugenzi na wakuu wa Idara za Utawala na
Rasilimaliwatu unaofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Selemani Mkomi.
***************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) imepata tuzo ya mshindi wa pili kundi la hospitali
kwenye usimamizi bora wa rasilimali watu.
Tuzo hiyo imetolewa na Ofisi ya
Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano mkuu wa
wakurugenzi na wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu uliomalizika
jana jijini Dodoma.
Akitoa tuzo hiyo Naibu Waziri
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sanga
aliipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwa na utendaji mzuri wa
kazi na kusimamia vizuri rasilimali watu .
"Nawapongeza kwa kuwa
washindi wa pili katika kundi la Hospitali kwenye masuala ya usimamizi bora na
mzuri wa rasilimali watu", alisema Mhe. Sanga.
Akizungumza mara baada ya
kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu cha Taasisi
hiyo Abdulrahman Muya aliishukuru Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora kwa kuona jinsi JKCI inavyofanya kazi kwa kufuata sheria,
kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
"Tunaahidi kuendelea
kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria,
kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali kupitia Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lakini pia kulinda
haki, wajibu na stahiki za wafanyakazi", alisema Muya.
Comments
Post a Comment