Upimaji na matibabu ya moyo bila malipo wilaya ya Handeni mkoani Pwani
*****************************************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni
na Taasisi ya Marafiki wa Maendeleo Handeni (MMAHA) tutatoa huduma za tiba
mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services
kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Wilaya ya Handeni
iliyopo mkoani Tanga.
Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote
yale kwa watoto na watu wazima tarehe 16 - 19/12/2024 saa 2:00 asubuhi hadi saa
10:00 jioni katika Hospitali ya Wilaya (Bomani) iliyopo Handeni Mjini (tarehe 16-17/12/2024) na Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni iliyopo Mkata – Mbweni (tarehe 18-19/12/2024.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa
elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa
maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa
yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo
watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya
kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga
jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba
wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo
ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana kwa simu namba 0713420242, 0717543823 na 0716601934.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu
Letu”.
Comments
Post a Comment