Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo bila malipo tarehe 09/12/2024
*********************************************************************************************************************************************************************************************************************
Katika
kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 09/12/2024 Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group tutatoa
huduma za tiba mkoba zijulikanazo
kwa jina la Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi.
Upimaji
huu utafanyika bila malipo yoyote yale kwa watoto na watu wazima tarehe 09/12/2024
kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu ya
lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha
na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanayoweza kuepukika
kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo wataanzishiwa matibabu hapohapo hii ikiwa ni pamoja na kupewa dawa za kutumia bila malipo yoyote yale.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754578190, 0783922571 na 0674179036
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.
Comments
Post a Comment