Watu 182 wajitokeza kupima moyo maadhimisho siku ya Uhuru wa Tanganyika



Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa  maadhimisho ya  siku ya Uhuru wa Tanganyika.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Joyce Manyama akimpima kiwango cha Oksijeni mwilini mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kupima afya ya moyo wake wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mlagwa Yango akizungumza na mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo leo kwaajili ya kupima afya ya moyo wake wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.


Fundi Sanifu wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Eliza Shuma akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwananchi aliyejitokeza kupima moyo wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Ashe Abillah akimpima uwiano wa urefu na uzito mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Efrem Ngaleka akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika katika taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika chumba cha daktari kwaajili ya kupata huduma za matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika.

********************************************************************************************************************************************************************************************************************

Watu 182 wamepata huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi maalumu ya upimaji iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group ikiwa ni maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.

Upimaji huo umefanyika leo bila malipo yoyote yale katika hospitali hiyo iliyopo TAZARA jijini Dar es Salaam ambapo watu wazima waliopata huduma walikuwa 147 na watoto 35.

Akizungumza kuhusu upimaji huo Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu alisema kati ya watu wazima 147 walioonwa 72 walikutwa na matatizo mbalimbali ya moyo ikiwemo shinikizo la juu la damu, matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kutanuka kwa kuta za moyo.

Dkt. Shemu alisema watoto walioonwa walikuwa 35 kati ya hao watano walikuwa na matatizo ya matundu kwenye moyo na mishipa ya damu ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake.

“Wananchi waliofika hapa wamepata huduma za kupima uwiano baina ya urefu na uzito, wingi wa sukari kwenye damu, shinikizo la damu, mfumo wa umeme wa moyo, jinsi moyo unavyofanya kazi, wamepata ushauri wa lishe bora na wale waliokutwa na matatizo tumewapa dawa za kwenda kutumia”.

 “Kupitia kambi hii maalumu ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika kama rais wetu alivyosema iwe ni siku ya kufanya shughuli za kawaida na kulinda afya nasi tukaona kulitekeleza hilo kwa vitendo  kwa kutoa huduma kwa wananchi bila gharama zozote zile”, alisema Dkt. Shemu.

Dkt. Shemu ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kupitia kambi hiyo mwitikio umekuwa mkubwa kwani sasa hivi jamii inafahamu umuhimu wa kuchunguza afya zao pamoja na kuishi maisha ambayo yatawawezesha kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliofika katika kambi hiyo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa za uchunguzi wa afya kwa wananchi wa Tanzania.

Alex Kahela mkazi wa Arusha alisema alipata bahati ya kuudhuria kliniki ya moyo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kukutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu aambapo wataalamu walimpatia dawa na kushauriwa kuendelea kufanya uchunguzi wa mara kwa mara.

Kahela alisema baada ya kumaliza dawa zile aliamua kufika Dar es Salaam kwaajili ya kufuatilia hali yake na kabla hajafika JKCI akakutana na kambi hiyo ya siku ya Uhuru hivyo kubahatika tena kwa mara ya pili kufanyiwa uchunguzi pamoja na kupata dawa bila gharama.

“Kwakweli namshukuru sana rais wangu kuwezesha kambi hizi za matibabu kwani zinatusaidia sisi watu wa hali ya chini kupata huduma. Nakumbuka kule Arusha nilikutwa na shinikizo la damu la 300 kwa 150, nilikuwa najisikia vibaya lakini kwasababu sikuwa na uwezo wa kwenda hospitali nilikuwa naishi tu hivyo hivyo”, alisema Kahela.

Kahela aliwaomba wataalamu wa afya wa JKCI kuendelea kuwafikia wananchi wa hali ya chini ili nao waweze kupata huduma kwa wakati kwani kwa hali aliyokuwa nayo Arusha kama asingepata matibabu labla leo asingekuwa hai.

Naye Mariam Lema mkazi wa Dar es Salaam alisema amewahi kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo huko nyuma lakini baada yakusikia JKCI inatumia siku ya Uhuru kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo akaona naye atumie fursa hiyo kupima kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

Mariam alisema hivi sasa maradhi  yamekuwa mengi hivyo ni muhimu kwa jamii kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili pale changamoto inapojitokeza iwe rahisi kutibika ikiwa ni katika hatua za mapema.

Mariam amewaomba wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ya kuondoa hofu ili waweze kuzitumia kambi za matibabu  ya magonjwa mbalimbali kufanya uchunguzi wa afya na kupokea majibu yao bila ya kuwa na hofu.

“Watu wengi wamekuwa na hofu ya kufanya uchunguzi wa afya kwamba wakikutwa na magonjwa haya makubwa maisha yao yatakuwaje na hivyo kugundulika wakiwa katika hali mbaya inayopelekea usugu na wakati mwingine kupoteza maisha”, alisema Mariam.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)