Mkazi wa Temeke apongeza huduma za upasuaji wa moyo alizofanyiwa JKCI
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agness Samuel akiangalia mapigo
ya moyo ya mgonjwa Jonathan Mwanayongo aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa
ya damu ya moyo bila kusimamisha moyo na wataalamu wa JKCI wakishirikiana na
wenzao kutoka Hospitali ya Jaslok ya nchini India.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Samuel akimuhudumia
mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya moyo bila
kusimamisha moyo Jonathan Mwanayongo. Mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji huo na
wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Jaslok ya
nchini India.
***************************************************************************************************
Mkazi wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Jonathan Mwanayongo ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kufanikisha upasuaji mkubwa wa moyo uliokuwa ufanyike nchini India.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari hii Jonathan alisema amegundulika kuwa na matatizo la moyo mwaka
huu na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya alibainika kuwa alikuwa na tatizo
la kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo iliyohitaji upasuaji wa haraka ili kuokoa
maisha yake.
Jonathan
alisema baada ya kufikishwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
alipokelewa na timu ya wataalamu mabingwa bobezi ambao walimfanyia uchunguzi wa
kina na kuanza maandalizi ya matibabu kabla ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa
moyo ulioshirikisha madaktari bingwa kutoka JKCI na Hospitali ya Jaslok ya
nchini India.
“Ulikuwa
ni upasuaji mkubwa ambao kwa kweli hatukuamini kama ungeweza kufanyika hapa
Tanzania hivyo nilikuwa nimeanza kufanya mpango wa kwenda nje ya nchi lakini
baada ya kukutana na wataalamu wa JKCI walinishauri kuwa matibabu hayo
yanafanyika hapa nchini na kweli
nimefanyiwa upasuaji na sasa naendelea vizuri”, alisema Jonathan.
Jonathan
aliongeza kuwa kwa sasa anaendelea vizuri kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji
huo na kwamba ameridhishwa na huduma alizopata katika Taasisi hiyo ikiwemo
huduma za wauguzi, madaktari na wataalamu wengine wote waliomhudumia.
“Nawaomba
watanzania wenzangu tusiwe na sababu za kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu
ya moyo kwani huduma hizi zipo hapa nchini na JKCI inafanya vizuri katika
kuhakikisha inaokoa maisha ya watanzania”, alisema Jonathan.
Jonathan
amewashukuru madaktari, wauguzi na watumishi wa JKCI kwa huduma bora na
kujitolea kwao akisisitiza kuwa taasisi hiyo ina uwezo mkubwa wa kutoa huduma
za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi katika matibabu ya moyo nchini.
.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment