JKCI yasaini makubaliano na China ujenzi wa hospitali mpya ya moyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Kiongozi wa kamati ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi kutoka Jamhuri ya Watu wa China Yang Ling wakionesha hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya moyo mara baada ya kusaini hati hiyo jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Kiongozi wa kamati ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi kutoka Jamhuri ya Watu wa China Yang Ling wakisaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya moyo jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa JKCI pamoja na wataalamu wa mradi wa ujenzi kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya moyo jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika ya Kusini na Mashariki, Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kiuchumi (AIEC) chini ya Wizara ya Biashara ya China Li Qing akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya ya moyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wataalamu wa mradi wa ujenzi kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali ya moyo iliyofanyika jana  katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa kamati ya ukaguzi wa mradi kutoka Jamhuri ya Watu wa China Yang Ling mara baada ya hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya moyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika ya Kusini na Mashariki, Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kiuchumi (AIEC) chini ya Wizara ya Biashara ya China Li Qing wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya ya moyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika ya Kusini na Mashariki, Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Kiuchumi (AIEC) na wataalamu wa mradi wa ujenzi kutoka Jamhuri ya Watu wa China  wakati wa hafla fupi ya kusaini  hati ya makubaliano ya ujenzi wa hospitali mpya moyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Na JKCI

***************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Wataalamu kutoka China wasaini hati ya makubaliano ujenzi wa hospitali mpya ya moyo itakayoleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa wagonjwa wa moyo nchini.

Hati hiyo imesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge pamoja na Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Mradi kutoka Jamhuri ya Watu wa China Yang Ling na kuahidi kuanza mchakato wa ujenzi huo mara baada ya taratibu kukamilika.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema hospitali hiyo itasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya kibingwa, pamoja na kuimarisha mazingira ya kazi kwa wataalamu wa afya wanaofanya kazi katika Taasisi hiyo.

“Mradi huu ni hatua muhimu sana katika kuimarisha uwezo wetu wa kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa viwango vya juu zaidi na kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma bora kwa wakati”, alisema Dkt. Kisenge

Dkt. Kisenge alisema mradi huo ni sehemu ya juhudi ya Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya afya na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.

 

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi