Kwa mara ya kwanza abiria wanaosafiri na treni ya SGR kunufaika na huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo itakayofanywa kwa abiria wanaotumia treni ya SGR katika kuadhimisha siku ya moyo duniani.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo itakayofanywa kwa abiria wanaotumia treni ya SGR katika kuadhimisha siku ya moyo duniani


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa  katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo itakayofanywa kwa abiria wanaotumia treni ya  SGR katika kuadhimisha siku ya moyo duniani.

Picha na JKCI

***********************************************************************************                                                 **********************************

Kwa mara ya kwanza abiria wanaosafiri na treni ya SGR kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonywa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo ndani ya treni.

Huduma hizo zitatolewa katika kambi maalumu itakayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha  siku ya moyo duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema abiria watanufaika na uchunguzi huo bila malipo kuanzia tarehe 21 hadi 27 Septemba mwaka huu.

 “Upimaji huo utafanyika kwa kutumia mashine zinazotumia akili unde ambapo abiria watapimwa kiwango cha sukari kwenye damu, uwiano wa uzito na urefu, shinikizo la damu (BP), kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) pamoja na kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electocadiography-ECG)”, alisema Dkt. Kisenge

Aidha Dkt. Kisenge aaliwataka wananchi na abiria kwa ujumla kutumia fursa hiyo ya kipekee kupima afya zao ili wsweze kuepuka gharama ambazo wangeweza kuzitumia kama wangefanyiwa vipimo hivyo Hospitalini.

“Kwa watu ambao wamekuwa wakisafiri mara kwa mara na kukosa nafasi ya kufika katika vituo vya afya ni vema wakatumia fursa hii kwani watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu na wale watakaohitaji majitabu zaidi tutawqpa rufaa ya kufika katika taasisi yetu kwaajili ya uchunguzi zaidi”, alisema Dkt. Kisenge

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa alisema abiria wengi watanufaika na zoezi hilo kutokana na idadi kubwa ya wasafiri wanaohudumiwa na shirika hilo kwa siku.

“Abiria zaidi ya 12000 husafiri kila siku hivyo kupitia kambi hii wananchi watanufaika na huduma za matibabu na kuweza kufahamu hali zao za afya”, alisema Mha. Shiwa

Mhandisi Shiwa alisema JKCI na TRC wana mpango wa kuwa na hospitali inayotembea katika treni ya SGR, hii itasaidia kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa wanaosafirishwa umbali mrefu kwa kutumia magari ya wagonjwa (Ambulance).


Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma