Wananchi wapata huduma za kibingwa za matibabu ya moyo Sabasaba
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abderehmani Njale akiwafundisha namna ya kumhudumia mgonjwa anayehitaji huduma ya dharura raia wa India waliofika katika banda la JKCI lililopo katika Banda la Jakaya Kikwete wakati wa Maonesho ya Sabasaba. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza afisa lishe wa Taasisi hiyo Husna Faraji alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika Banda la Jakaya Kikwete wakati wa maonesho ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Afisa huduma bora kwa wateja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau akimwelezea mwananchi aliyefika katika banda la JKCI lililopo katika Banda la Jakaya Kikwete huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Irene Mdingi kimpima shinikizo la damu mwananchi aliyetembelea banda la JKCI lililopo Banda la Jakaya Kikwete katika maon...