Pemba wajitokeza kwa wingi kupimwa na kutibiwa moyo


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce akimweleza mkazi wa Pemba umuhimu wa kutumia dawa za moyo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya  siku tano inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba.


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eveline Furumbe akimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo  siku tano inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba. 

Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabella Mkojera akimuuliza maswali ya uelewa wa magonjwa ya moyo mkazi wa Pemba aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba kwaajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali hiyo.

Baadhi ya wananchi waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali hiyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano.


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa