Tanzania yafanya upasuaji wa moyo nchini Zambia



Madaktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimlaza mgonjwa kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Upasuaji huo umefanyika hivi karibuni nchini Zambia ambapo wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali ya Moyo Zambia walifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye chumba cha juu upande wa kushoto wa moyo (Myxoma). Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel ndilo lililoratibu ufanyikaji wa upasuaji huo. 


Wataalamu wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kwa watoto  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa   kuondoa uvimbe kwenye chumba cha juu upande wa kushoto wa moyo (Myxoma).Upasuaji huo umefanyika hivi karibuni nchini Zambia ambapo wataalamu wa JKCI walifanya upasuaji  kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali ya Taifa ya Moyo ya Zambia. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel ndilo lililoratibu ufanyikaji wa upasuaji huo. 


Daktari bingwa wa wagonjwa wa dharura na mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Vivian  Mlawi akiwafundisha wataalamu wa afya wa  Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi wakati wataalamu wa JKCI walipokwenda katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanya upasuaji wa moyo na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel ndilo lililoratibu ufanyikaji wa upasuaji huo. 


Wataalamu  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia, Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel na Congenital Heart Academy kutoka nchini Italia wakiwa katika kikao cha kuangalia ni namna gani JKCI itakavyowajengea uwezo wataalamu wa hospitali hiyo  ili waweze kutoa huduma za upasuaji wa moyo.


Wataalamu  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia, Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel na Congenital Heart Academy kutoka nchini Italia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa  kikao cha kuangalia ni namna gani JKCI itakavyowajengea uwezo wataalamu wa hospitali hiyo  ili waweze kutoa huduma za upasuaji wa moyo.




Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)