Dkt. Kisenge: Jengeni tabia ya kupima magonjwa ya moyo mara kwa m
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wananchi waliofika katika Kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kupata huduma katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo. Mkurugenzi wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akielezea tatizo la magonjwa ya moyo lilivyo duniani wakati wa kuadhim...