JKCI yatoa huduma ya matibabu ya moyo Sabasaba
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiangalia jinsi Daktari kutoka Hospitali ya JKCI Dar Group Samweli Mbilinyi anavyotoa huduma ya dharura kwa wagonjwa alipotembelea banda la Taasisi hiyo leo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wataalamu wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea banda la Hospitali hiyo leo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Afisa Uuguzi wa chumba cha uchunguzi na matibabu ya upasuaji mdogo wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Flora Kasembe akiwaonesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo betri la moyo (pacemaker) wanalowekewa wagonjwa ambao mapigo ya mioyo yao iko chini ya asilimia 50 wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Afisa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anuwarite John akiwa...