Makonda aishukuru JKCI kwa kufanya upimaji wa moyo kwa wakazi wa Arusha

 

Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rose Chengo akimweleza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kuhusu watoto wanaotibiwa katika kambi maalum ya madaktari bingwa na wabobezi wa magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akimsalimia mwananchi aliyefika kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa  kambi maalum ya madaktari bingwa na wabobezi wa magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akisalimiana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce anayetoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa huo zinazotolewa katika kambi maalum ya madaktari bingwa na wabobezi wa magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Kambi hiyo ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali imeratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

*********************************************************************************************************************************************************************************************

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewashukuru wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi wa mkoa huo  kupitia kambi maalumu ya madaktari bingwa na wabobezi wa magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Pongezi hizo amezitoa jana  alipotembelea kambi hiyo ya matibabu iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Makonda alisema mchango wa taasisi hiyo wa kuboresha afya za wananchi wa Arusha ni wa kipekee kwa kuwa imewasaidia watu wengi  kupata huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo ambazo ilibidi  wasafiri na kuzifuata jijini  Dar es Salaam.

“Ninawashukuru madaktari kwa moyo wa kujitoa waliouonyesha kwa wananchi wa Arusha na ninawapongeza kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya”, alisema Makonda.

Makonda alitumia fursa hiyo pia kuwaaga madaktari wa JKCI na kuwaomba waendelee kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi bila ya kuangalia tofauti ya vipato vyao.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloyce Mohamed alimshukuru Makonda kwa moyo wake wa kujitoa wa kuhakikisha wananchi wa Arusha wanapata huduma bora za matibabu ya moyo.

Kambi hiyo ya siku saba inalenga kutoa huduma za upimaji na ushauri wa kitaalamu wa magonjwa ya moyo kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha na mikoa jirani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya serikali ya kuhamasisha utunzaji wa afya.

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa