JKCI yaelezea teknolojia inazozitumia wakati wa Kongamano la Kisayansi la MUHAS
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Albert Msando alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa Kongamano la 13 la kisanyansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika hivi karibuni katika chuo hicho kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akimpatia moja ya kipeperushi
kinachoelezea huduma zinazotolewa na Taasisi
hiyo Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Albert Msando alipotembelea banda la taasisi
hiyo wakati wa Kongamano la 13 la kisanyansi
la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika
hivi karibuni katika chuo hicho kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wa Kongamano la 13 la kisanyansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika hivi karibuni katika chuo hicho
kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Na: Jeremiah Ombelo
*****************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeelezea inavyotumia
teknolojia ya tiba mtandao (Telehealth) katika kuboresha huduma za afya inazozitoa
kumsaidia mgonjwa kuwasiliana na daktari popote alipo.
Hayo yameeleza na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya wakati wa Kongamano la 13 la Kisayansi la
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililokuwa
likifanyika katika kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam na kumalizika
hivi karibuni.
Taasisi hiyo pia imeeleza jinsi inavyotumia teknolojia kwa kutumia
kifaa kijulikanacho kwa jina la Dozee kufuatilia hali ya mgonjwa akiwa nyumbani
kwa kufuatilia mzunguko wa damu, shinikizo la damu na mapigo ya moyo.
“Tupo katika kongamano hili la kisayansi kuwapa elimu wadau wa
afya namna ambavyo JKCI inatumia teknolojia katika masuala ya Tiba mtandao
(Telehealth) na huduma za kuchunguza hali ya mgonjwa aliyopo nyumbani kwa
kutumia kifaa cha Dozee”, alisema Dkt. Angela.
Dkt. Angela alisema katika kongamano hilo wataalamu wa afya
wameweza kujadili mada mbalimbali ikiwemo machapisho na tafiti zilizofanywa na
wataalamu wa JKCI kupitia MUHAS ambazo zimetoa matokeo yenye mchango mkubwa uliofanyika
katika sekta ya afya.
“Moja ya mafanikio makubwa yaliyojadiliwa kwenye kongamano hilo ni
pamoja na uzinduzi rasmi wa Kituo cha Taifa cha Tafiti na Matibabu ya Mishipa ya Damu na
Magonjwa ya Moyo (Centre of Excellence for East and Central Africa)”,
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa alioufanya katika
kufanikisha uanzishwaji wa kituo hiki muhimu cha Tafiti na Matibabu
ya Mishipa ya Damu na Magonjwa ya Moyo (Centre of Excellence for East and
Central Africa)” alisema Dkt. Muhozya.
Kwa upande wake Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Samweli Msigwa alieleza kuwa JKCI ina teknolojia zinazoweza kuokoa maisha pale
ambapo mgonjwa anakuwa kwenye hali inahohitaji huduma ya dharura na haraka.
“Tunatumia teknolojia kutoa huduma kwa wagonjwa wetu ambapo kwa
kutumia kifaa cha Dozee kinachotuwezesha kutoa huduma ya haraka na
kuokoa maisha ya mgonjwa pale inapotuonyesha mzunguko wa damu ya mgonjwa,
shinikizo la damu na mapigo ya moyo ya mgonjwa haviko sawa,”
“Upande wa huduma ya Telehealth wagonjwa
wetu wanaweza kuzungumza na dakatari kwa njia ya mtandao, kupata
ushauri wa kitaalamu, kuandikiwa vipimo na dawa bila kufika hospitalini kwani
kinachohitajika kufanikisha huduma hii ni simu janja ama kompyuta kwaajili ya
kuweka miadi na kuonana na daktari mtandaoni”, alisema Dkt. Msigwa.
Comments
Post a Comment