Wachezaji nchini kupimwa moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya programu ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo nchini jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wakibadilishana hati ya makubaliano ya programu
ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo nchini wakati wa hafla ya kusaini hati hiyo
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wakisaini hati ya makubaliano ya programu
ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo nchini wakati wa hafla ya kusaini hati hiyo
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya program ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo nchini iliyofanyika jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
**********************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yazindua programu ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo nchini.
Programu hiyo imezinduliwa jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kuanza kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars).
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema programu hiyo ijulikanayo kwa jina la Kadiolojia ya michezo imelenga kulinda afya za mioyo ya wanamichezo nchini.
“Programu hii ni ya kipekee na ya kwanza hapa nchini, itatoa huduma kwa wanamichezo wa ngazi ya kitaifa na ngazi zingine za michezo, wanajeshi wanaofanya mazoezi kila siku pamoja na watoto wa shule wanaoanza safari yao ya michezo”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema uanzishwaji wa progamu hiyo ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha michezo na kuunganisha taifa na mataifa mengine kupitia michezo.
“Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha michezo inafanyika kwa hamasa katika ngazi za kitaifa na kimataifa hata kuanzisha kampeni ya goli la mama, sisi hatuna budi kumuunga mkono kwa kuhakikisha wanamichezo wetu wana afya bora ya mioyo yao na kuzuia vifo vya ghafla vinavyoweza kusababishwa na mshtuko wa moyo wa ghafla wawapo uwanjani”,
“Takwimu zinaonyesha kuwa takribani mchezaji mmoja kati ya 50,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tatizo hilo, wengine hushindwa hata kufika hospitalini na mara nyingi vifo hivi hutokea mbele ya mashabiki kwenye viwanja vya michezo na huacha jamii ikiwa katika huzuni na mshangao”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake
Rais wa Shirikisho la Mpiara wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema kwa
muda mrefu kumekuwa na changamoto kubwa ya vijana hasa mashuleni na katika
timu za mitaani kupoteza maisha ghafla uwanjani kutokana na matatizo ya moyo ambayo
hayajawahi kugunduliwa mapema.
Kwa
kutambua hilo TFF pamoja na Chama cha Makadtari wa Michezo Tanzania wameungana rasmi na
JKCI katika kuanzisha na kusimamia kwa pamoja Programu ya upimaji wa magonjwa
ya moyo kwa wanamichezo wakiwemo wa ligi kuu na ligi daraja la
kwanza.
Wallace
alisema Progarmu hiyo itahusisha mafunzo maalum kwa madaktari wa timu na
wataalamu wa afya kuhusu magonjwa ya moyo yanayohusiana na michezo na kutimiza
ndogo ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa kipindi kirefu katika historia ya michezo
nchini.
“Tanzania
tunajiandaa kwa mashindano makubwa – CHAN 2025 na AFCON 2027, ambayo ni nafasi ya kipekee kwa taifa
letu kuonesha uwezo wake katika kandanda na pia kuwekeza katika afya ya
wachezaji wetu. TFF inatambua kuwa mafanikio katika michezo hayawezi kupatikana
bila kuwa na wachezaji wenye afya bora hasa afya ya moyo”, alisema Wallace
Wallace
alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka
Duniani (FIFA) wamekuwa wakisisitiza juu ya umuhimu wa
uchunguzi wa moyo kabla ya wachezaji kushiriki mashindano yoyote, hii ikiwa ni
sehemu ya sera za kimataifa za ulinzi wa maisha ya wachezaji.
“Sisi
kama TFF, hatuwezi kubaki nyuma, tunajiunga na vyama vyote vya mpira duniani
katika utekelezaji wa sera hii na kuanzisha sera mpya kua kila mwanamichezo
kabla ya kujiunga na michezo lazima achunguzwe afya ya moyo nakuendelea
kuchunguzwa kwa vipindi tofauti na hii ifanyike kwa ngazi zote hadi mashuleni”,
alisema Wallace
Comments
Post a Comment