JKCI yatoa huduma ya matibabu ya moyo Sabasaba

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiangalia jinsi Daktari kutoka Hospitali ya JKCI Dar Group Samweli Mbilinyi anavyotoa huduma ya dharura kwa wagonjwa alipotembelea banda la Taasisi hiyo leo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wataalamu wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea banda la Hospitali hiyo leo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa chumba cha uchunguzi na matibabu ya upasuaji mdogo wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Flora Kasembe akiwaonesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo betri la moyo (pacemaker) wanalowekewa wagonjwa ambao mapigo ya mioyo yao iko chini ya asilimia 50 wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Afisa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anuwarite John akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo huduma zinazotolewa na JKCI wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Wananchi wakichagua bidhaa mbalimbali zinazouzwa na Shirika lisilo la  Kiserikali la Heart Team Africa Foundation (HTAF) kwaajili ya kuchangia matibabu ya moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Picha na: JKCI

 *****************************************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa