Waziri Mkuu Majaliwa aishauri JKCI kufungua matawi nje ya nchi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa
Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) unaofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa (AICC) Arusha.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakizungumza na wadau wa sekta ya afya waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimpatia zawadi ya picha kutoka Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) daktari bora wa mwaka ambaye ni bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) unaofanyika jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Godwin Mollel akiwasili katika
viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) na kupokelewa na viongozi
kutoka Taasisi za Afya wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha
Madaktari Tanzania (MAT) unaofanyika jijini Arusha.
Picha na: JKCI
**********************************************************************************************
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa aishauri Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuangalia
uwezekano wa kufungua matiwi ya Taasisi hiyo nje ya nchi.
Hayo ameyasema leo alipotembelea banda la Taasisi hiyo
wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Mkuu wa
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Arusha, jijini Arusha.
Mhe. Majaliwa alisema JKCI sasa inafanya vizuri na
imesaidia kuipunguzia Serikali gharama ya kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa
nje ya nchi kwani sasa huduma nyingi za matibabu ya moyo zinapatikana hapa
nchini.
“Hongereni sana kwa huduma nzuri mnayoitoa kwa
wagonjwa wa moyo, JKCI sasa ni jicho la nchi katika masuala ya matibabu ya moyo
kwa kuimarisha huduma zake na kuwapa unafuu wagonjwa wa moyo kupata huduma
kirahisi, angalieni namna ya kupeleka huduma hizi nje ya mipaka ya Tanzania kwa
kufungua matawi yenu”, alisema Mhe. Majaliwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba kutoka Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane alisema Taasisi hiyo imefanikiwa
kufanya tiba utalii kwa kufanya kambi maalumu za matibabu ya moyo katika nchi
za Comoro, Malawi na Zambia.
“Taasisi yetu imekuwa ikiwafikia wananchi wengi katika
mikoa mbalimbali nchini kwa kufanya kambi maalumu za matibabu ya moyo pia tumeweza
kuvuka mipaka ya Tanzania lengo likiwa kuimarisha tiba utalii nchini”, alisema
Dkt. Waane
Dkt. Waane alisema Taasisi hiyo pia imeweza
kuwasogezea huduma karibu wananchi kwa kufungua matiwi yake maeneo maeneo ya
Kawe ili kuwapunguzia msongamano wa kupata huduma za matibabu ya moyo katika
eneo moja.
Kwa kipindi cha miaka mnne Taasisi hiyo imeweza kuwapatia
matibabu wagonjwa 689 kutoka nje ya nchi zikiwemo nchi za Somalia, Malawi,
Kenya, Rwanda, Nigeria, Siera Leon, Zimbambe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia,
Burundi, na wengine kutoka nje ya Afrika katika nchi za Armenia, china,
Ujerumani, India, Norway, Ufaransa na Uingereza.
Comments
Post a Comment