Posts

Showing posts from 2026

JKCI yawahamasisha Wananchi kujitokeza kupima Afya Kariakoo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya upimaji wa afya bila malipo inayofanyika   katika kliniki ya Taasisi hiyo iliyopo Soko kuu la Kariakoo ghorofa ya tano. Wananchi wakisubiri kupata huduma ya matibabu ya magonjwa mbalimbali wakati wa kambi maalum ya upimaji wa afya inayofanyika bila malipo katika  Tawi la  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  lililopo Soko Kuu la Kariakoo ghorofa la tano jiji Dar es Salaam. Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group, Joachim Mvungi akitoa elimu ya jinsi ya kupiga mswaki kwa wananchi waliofika katika kambi maalum ya upimaji wa afya bila malipo inayofanyika katika    Kliniki ya JKCI Soko Kuu la Kariakoo ghorofa la tano jiji Dar es Salaam.  Daktari bingwa wa Macho wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group, Fe...

JKCI Yatoa Rai kwa Watumishi Kuongeza Ufanisi na Weledi Kazini

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa JKCI jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akichangia mada wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga akiwasilisha taarifa ya fedha  ya mapato na matumizi ya  taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Mbaruku akichangia mada wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa JKCI iliyopo jiji...

Afya kwanza! JKCI Dar Group yawafikia watu 527 Kijichi

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimjulia hali bibi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizika hivi karibuni Kijichi wilaya ya Temeke na. Zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Steven Kihoko akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizka hivi karibuni  Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Abderahman Njale akimpima mfumo wa umeme wa moyo mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizka hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ...

Wafanyakazi 121 wa TANAPA wapimwa Afya ya Moyo Arusha

Image
Afisa Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Mndasha     akimueleza mfanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) huduma zinazotolewa na taasisi hiyo wakati wa zoezi la upimaji afya ya moyo kwa wafanyakazi wa TANAPA ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Aim Sports mkoani Arusha. Daktari wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) inayosimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Advotus Kimomogoro akimsikiliza mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Aim Sports kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa afya ya moyo iliyokuwa inatolewa kwa wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Matroni wa Hospitali ya  Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) inayosimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Florah Kasembe akimkabidhi zawadi Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAP...

JKCI na Watalaamu wa Ujerumani waokoa Maisha ya watoto 15

Image
Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Moyo Mission ya nchini Ujerumani wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu la moyo katika kambi maalumu ya siku tano ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanyika JKCI ambapo watoto 15 walifanyiwa upasuaji. Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalumu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Loth na daktari bingwa wa moyo kwa watoto kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Moyo Mission ya nchini Ujerumani Harms Sebastian wakimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mtoto ambaye moyo wake una tundu  wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanyika JKCI. Wataalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi (Heart Lung Machine) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Moyo Mission ya nchini Ujerumani wakiendesha mas...

Kamati ya Bunge yapongeza uwekezaji wa Mhe. Rais Dkt. Samia JKCI, yasema waongeza nguvu ya matibabu ya Moyo nchini

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI walipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa pamoja na uwekezaji uliofanywa na Serikali. Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Dkt. Johannes Lukumay akimjulia hali mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wakati kamati hiyo ilipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na uwekezaji uliofanywa na Serikali. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naizihijwa Majani akiwaelezea wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI huduma zinazotolewa kwa watoto aliolazwa katika wodi ya wagonjwa watoto wanaohitaji uangalizi maalumu (PICU)wakati kamati hiyo ilipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na uwekezaji ul...

Jamii yahimizwa kupima Afya mara kwa mara kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza

Image
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku tatu inayofanywa na Hospitali hiyo katika eneo la Kijichi wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Daktari wa kinywa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Joachim Mvungi akichunguza kinywa cha mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku tatu inayofanywa na Taasisi hiyo jana Kijichi wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dorica Salustianus akimsikiliza mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya inayofanywa na wataalamu wa Hospitali hiyo kwa wakazi wa Kijichi wilaya ya Temeke na maeneo ya jirani. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Irene Ngowi akimuelezea umuhimu wa kufuata mtindo bora wa maisha mwan...

Serikali yamuokoa Mama wa Kivule kwa matibabu ya moyo ya shilingi milioni 29 JKCI

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zaina Mlingo akimpima shinikizo la damu Mama Anna Mwansasu mkazi wa Kisamvule jijini Dar es Salaam ambaye amefanyiwa upasuaji mdogo wa kupandikiziwa   kifaa cha CRT (Cardiac Resynchronization Therapy) ambacho kinausaidia moyo kupiga mapigo yake kwa mpangilio sahihi. Gharama ya matibabu hayo ni zaidi ya shilingi  milioni 29 ambapo serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imelipia. ***************************************************************************************************************************************************************************************************** Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam Mama Anna Mwansasu , ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumsaidia kugharamia matibabu ya kubadilishiwa kifaa cha CRT (Cardiac Resynchronization Therapy) ambacho kinausaidia moyo kupiga mapigo yake kwa mpangilio sahihi...