JKCI yawafanyia uchunguzi wa afya wafanyakazi 134 wa Bohari ya Dawa (MSD)
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Edward Martin akizungumza na mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Doreen Josiah mara baada ya kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku ya mbili iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka JKCI na kumalizika jana katika Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Daniel Munishi akimpima wingi wa sukari katika damu mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Ziada Athumani wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzuzi wa afya iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka JKCI na kumalizika jana katika Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima shinikizo la damu mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Peace Nyankojo wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzuzi wa afya iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka JKCI na kumalizika ja...