Shilingi Bilioni 8 yawekezwa JKCI-ALMC kuelekea AFCON 2027
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC) Peter Maduki na Mkurugenzi wa JKCI-ALMC Dkt. Tatizo Waane wakikagua wodi za wagonjwa mashuhuri (VIP Wards) zilizopo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Arusha
Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC) Dkt. Tatizo Waane akiwaonesha wadau maeneo
ya wodi za watu mashuhuri (VIP Wards) zilizopo katika Taasisi hiyo iliyopo
jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano na
waandishi hao kuelezea utayari wa JKCI-ALMC katika kutoa huduma bora za afya
kuelekea michuano ya AFCON 2027.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Arusha
Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC) Dkt. Tatizo Waane akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao kuelezea utayari wa JKCI-ALMC
katika kutoa huduma bora za afya kuelekea michuano ya AFCON 2027.
Na JKCI
*********************************************************************************************************************
Shilingi bilioni 8 zawekezwa
na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC)
kufanya ukarabati wa Hospitali hiyo, kununua vifaa tiba vya kisasa vinavyotumia
akili unde na kuanzisha huduma za vyumba vya wagonjwa mashuhuri (VIP Wards) kuelekea
mashindano ya AFCON 2027.
Uwekezaji huo umeenda
sambamba na uwekezaji wa smart device
ambazo JKCI-ALMC imejipanga kuweka katika hoteli mbalimbali zilizopo Arusha ili
wageni watakaofika nchini wawezi kufanya uchunguzi wa viashiria vya magonjwa ya
moyo wanapokuwa hotelini.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema vyumba vya VIP vilivyopo JKCI-ALMC vinaweza
kugeuzwa matumizi na kuwa vyumba vya uangalizi maalumu (ICU) pale hali ya
mgonjwa inapobadilika hivyo kuokoa maisha kwa wakati.
“Maboresho tunayoyafanya
katika Taasisi yetu yanaenda kuwasaidia wananchi wa kanda ya Kaskazini lakini
pia yataitambulisha nchi yetu kuwa na Taasisi ya afya yenye mazingira mazuri,
huduma bora za afya zenye hadhi ya kimataifa wakati wa mashindano ya AFCON
2027”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema JKCI
imejipanga kuweka wataalamu wake katika viwanja vitakavyotumika wakati wa
mashindano ya AFCON 2027 ili changamoto za kiafya zinapotokea katika michuano
hiyo huduma za afya zinatolewa kwa wakati na kuwawezesha mashabiki wa
mashindano hayo kupata huduma za uchunguzi wa afya wanapokuwa uwanjani.
Sambamba na maandalizi
yanayofanywa na JKCI-ALMC Dkt. Kisenge alisema shilingi bilioni 18 zimetengwa na
Serikali kwaajili ya ujenzi wa jengo litakalojengwa JKCI Hospitali ya Dar Group
kwaajili ya kutoa huduma za afya kwa wanamichezo
wa Afrika Mashariki na Kati.
Aidha Dkt. Kisenge
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya ikiwemo mpango wa kuwekeza
zaidi ya shilingi bilioni 20 JKCI-ALMC ili kuhakikisha huduma za afya kanda ya
kaskazini zinaimarika
“Uwekezaji huo utahusisha
ufungwaji wa mashine kubwa za kufanya uchunguzi wa afya ikiwemo CT Scan, mtambo
wa CathLab pamoja na MRI ambayo kwa Afrika Mashariki na kati ndio itakuwa MRI ya
kwanza kwa ukubwa”,
“Tunataka JKCI-ALMC kuwa
Hospitali ya kwanza Afrika Mashariki na kati kutumia mifumo ya kiautomatiki
katika kila hatua anayopita mgonjwa, na kwa kufanya hivyo tumeendelea kutekeleza
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo
Global Med Care katika kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa”, alisema Dkt.
Kisenge
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC)
Dkt. Tatizo Waane alisema uboreshwaji wa huduma za afya katika tawi la
JKCI-ALMC umechangia katika kuboresha afya za wagonjwa kupitia huduma bingwa
bobezi wanazozitoa.
“JKCI-ALMC ni moja ya
hospitali ambayo ilikaguliwa na kuona inafaa kutoa huduma za matibabu wakati wa
mashindano ya AFCON, matibabu tutakayotoa yatahusisha wananchi, wachezaji, na
mashabiki watakaokuja nchini”, alisema Dkt. Waane
Dkt. Waane alisema matibabu
yanayotolewa na JKCI-ALMC ni matibabu ambayo mgonjwa anaweza kuyapata mahali
popote duniani kutokana na uwekezaji mkubwa wa wataalamu, vifaa tiba vya kisasa
na ujuzi.





Comments
Post a Comment