Watu 689 wapimwa moyo Geita
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mwananchi wa Geita aliyefika katika banda la JKCI wakati wa maonyesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya madini yaliyomalizika leo Mkoani Geita. Jumla ya watu 689 wamepatiwa huduma katika banda hilo. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayetoa huduma katika kliniki maalumu Grace Mbanga akimpima shinikizo la damu mwananchi wa Geita aliyetembelea banda la JKCI wakati wa maonyesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya madini yaliyomalizika leo Mkoani Geita. Jumla ya watu 689 wamepatiwa huduma katika banda hilo. Afisa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Elimiliki Kileo akimpima urefu, uzito na uwiano wa urefu na uzito mkazi wa Geita aliyetembelea banda la JKCI wakati wa maonyesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya madini yaliyomalizika leo Mkoani Geita. Jumla ya watu 689 wamepatiwa huduma katika banda hilo. Wa...