Matibabu ya moyo yatolewa bure kwenye maonesho ya Madini Mkoani Geita
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi
(Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Geita wakati wa maonesho ya sita ya kimataifa
ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani
Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari
kwenye damu na shinikizo la damu katika maonesho hayo.
Wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wakiendelea
kupata huduma katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa
maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika
Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi na
matibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari kwenye damu na shinikizo la damu katika
maonesho hayo.
Picha na: JKCI
********************************************************************************************
Comments
Post a Comment