JKCI kutoa huduma bure siku ya moyo Duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya siku ya moyo duniani yatakayofanyika tarehe 29/09/2023 jijini
Dar es Salaam.
*************************************************************************************************************************************************************************************************
Na Aveline Kitomary
KATIKA Kuelekea
maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani Septemba 29 kila Mwaka Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Moyo
Tanzania wanatarajia kutoa huduma za upimaji bure katika Tawi la JKCI la Dar
Group Hospital iliyopo jijini Dar es Salaam.
Takwimu zinaonesha
takribani watu milioni 20 hupoteza maisha Duniani kutokana na magonjwa ya moyo
ambapo pia hapa nchini takribani asilimia 13 hupoteza maisha.
Akizungumza na Waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Moyo
Tanzania( TCS) ,Dk Roberth Mvungi amesema kambi maalum ya matibabu
itakayohusisha uchunguzi na utambulishi wa kujua viashiria vya magonjwa ya moyo
itafanyika kwa siku mbili Septemba 29 hadi 30,2023.
"Nchi yetu imepiga
hatua sana katika matibabu ya moyo na chama kimeona ni heri kushirikiana na
wadau wakubwa ambao wamehusika kubadilisha hadhi ya Tanzania katika kutibu na
kukinga magonjwa ya moyo,"aneeleza.
Amesema kutakuwa na
matembezi ambayo yataanza saa 12:00 asubuhi siku ya Septemba 30.
"Tutafanya
uchunguzi wa afya Dar group Hospital watu wote wanakaribishwa kuangalia na
kutambua afya yao na tuna matembezi maalum tutatembea kutoka uwanja wa uhuru
Chang'ombe Temeke hadi Tazara Dar Group.
Alifafanua kuwa asilimia
80 ya magonjwa ya moyo yananikingika endapo ushauri wa wataaamu utafatwa.
Kauli mbiu "Tumia
moyo, kulinda moyo wako".
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dk Peter Kisenge amesema
Kwa kushirikiana na chama kwa pamoja wanaadhimisha siku ya moyo Duniani ambapo
watapima wagonjwa matatizo ya moyo ambapo aliwaomba wananchi watoke majumbani
mwao kuja kupima magonjwa ya moyo.
"Serikali imejikita
kuimarisha afya tuna vifaa vya kisasa tutapima,madakatari bingwa watakuwepo
hivyo wananchi wajitokeze unapokuja mapema utapata matibabu mapema hautatumia
graharama na vipimo vitafanyika hadi siku ya Jumamosi na mazoezi yatafanyika ni
muhimu mazoezi kufanyika kwa wakati ili kujikinga,"amesisitiza Dk Kisenge.
Amesema watapima
kisukari,uzito na pia watatoa elimu ya lishe na wataaamu watakuwepo na
watawaeleza madhara ya sigara na unywaji pombe uliokithiri.
Amesema mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo atakuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert
Chalamila.
Comments
Post a Comment