Bulembo aipongeza JKCI kupeleka vipimo waliko wananchi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo akimsalimia mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwaajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni. Kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar Group Dkt. Tulizo Shemu. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo akiwasili katika viwanja vya Hospitali ya wilaya hiyo kwaajili ya kuangalia huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinatolewa na wataalamu ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali hiyo. Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar Group Dkt. Tulizo Shemu. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu kuhusu kambi maalumu ya upimaji na matiababu ya moyo inayofanywa na wataamu w...