Wataalamu wa JKCI wawasilisha utafiti walioufanya katika mkutano wa Kimataifa wa Kisayansi wa Magonjwa yasiyoambukiza
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akiwasilisha taarifa ya utafiti alioufanya kuhusu wanawake wanaopata magonjwa ya moyo kutanuka na kushindwa kufanya kazi kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy) wakati wa mkutano wa kimataifa wa kisayansi wa magonjwa yasiyoambukiza unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ifakara anayeshirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Neema Kailembo akiwasilisha taarifa ya utafiti alioufanya wa matokeo ya awali yaliyogawanya makundi tofauti ya viashiria hatarishi vinavyosababisha mishipa ya damu kwenye moyo kuziba wakati wa mkutano wa kimataifa wa kisayansi wa magonjwa yasiyoambukiza unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere.
Wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Janeth Mmari na Neema Kailembo wakimsikiliza mtaalamu wa afya kutoka Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) alipokuwa akiwaelezea kuhusu utafiti ulioufanyika KCMC kuhusu ugonjwa wa kiharusi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kisayansi wa magonjwa yasiyoambukiza unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere.
Comments
Post a Comment