JKCI kufanya upimaji na matibabu ya moyo wilayani Kigamboni


 Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

************************************************************************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Wilaya ya  Kigamboni tutatoa huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa  jina la  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 27/11/2023 hadi tarehe 01/12/2023  saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Viwanja vya Hospitali ya Wilaya Kigamboni iliyopo eneo la Gezaulole.

Kutakuwa na madaktari bingwa  wa moyo watakaoambatana na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

 Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0756284418 Dkt. Lucas Ngamtwa Mganga Mkuu Manispaa ya Kigamboni, 0786220116 Dkt. Mohamed Mnyau  Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Kigamboni na 0713327156  Chemere Sirira Mratibu wa Huduma za  Kitabibu Manispaa ya Kigamboni.

  “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari