Wakumbushwa madhara ya kutoa na kupokea rushwa


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kupata mafunzo ya kuzuia rushwa eneo la kazi. Mafunzo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mkuu wa uendeshaji umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Nerry Mwakyusa akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) madhara ya kutoa na kupokea rushwa kutoka kwa wananchi wanaopata huduma  katika Taasisi hiyo iliyopo  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa eneo la kazi yaliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).




Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari