20 kufanyiwa upasuaji wa moyo



 

Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka shirika la Open Heart International (OHI) lililopo nchini Australia kumfanyia upasuaji wa kufungua mlango wa moyo wa chini kushoto ulikuwa umeziba na kutopitisha damu vizuri mgonjwa mwenye matatizo ya valvu wakati wa kambi maalumu ya siku 4 iliyoanza leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya watu wazima 10 watafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo inayotoa huduma za matibabu pamoja na mafunzo kwa wataalamu wa afya wa JKCI.


Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirila la Open Heart International (OHI) lililopo nchini Australia kuziba tundu na kufungua mishipa ya damu iliyoziba (tof repair) wakati wa kambi maalumu ya siku 4 iliyoanza leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto 10 watafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo inayotoa huduma za matibabu pamoja na mafunzo kwa wataalamu wa afya wa JKCI.

Na:JKCI
***********************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa