Taarifa kwa wataalamu wa afya nchini

Wataalamu wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha Valvu iliyokuwa haipitishi damu vizuri.

 ********************************************************************************************************************************************************************************************************************

TAARIFA KWA WATAALAMU WA AFYA NCHINI

KAMBI MAALUMU YA UPASUAJI WA MISHIPA YA DAMU (AORTIC ANEURYSM STENTING)

 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalamu wa afya nchini kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa kuwapa rufaa ya kuja katika Taasisi yetu wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya mshipa mkubwa wa damu -Aorta kutanuka au kuchanika (AORTIC ANEURYSM au AORTIC DISSECTION) kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na upasuaji.

Matibabu haya yatatolewa na wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya BLK ya  nchini India katika kambi maalumu ya matibabu itakayofanyika  tarehe 13 hadi 17 Novemba 2023 jijini Dar es Salaam. Wataalamu hawa watawafanyia wagonjwa  watu wazima upasuaji  wa mishipa ya damu kwa njia ya tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Aneurysm Stenting).

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0685 110187 Dkt. Tryphone Kagaruki, 0716 696217 Dkt. Alex Joseph na 0788 308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

 “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini