Posts

Showing posts from October, 2025

Serikali yaokoa Mil.500 kwa Upasuaji wa moyo JKCI

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia tuzo ya shukrani  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mratibu wa Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia Darren Wolfers kutokana na ushirikiano uliopoa baina ya JKCI na shirika hilo katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watanzania na mafunzo kwa wataalamu wa afya. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza wakati wa kufunga kambi maalumu ya upasuaji wa moyo iliyofanywa na  wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa  Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia ambapo wagonjwa 17 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo. Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akitoa neno la shukrani wakati wa     kufunga kambi maalumu ya upasuaji wa moyo iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la O...

Viongozi wa JKCI Hospital ya Dar Group wajengewa uwezo wa kudhibiti viha...

Image

Viongozi wa JKCI Hospital ya Dar Group wajengewa uwezo wa kudhibiti vihatarishi vya kiutendaji

Image
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospital ya Dar Group wakimsikiza CPA. Cosmas Mbogela wakati akitoa  mafunzo ya jinsi ya  kutambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaji kazi wa hospitali hiyo yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospital ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu na Mkuu wa Kitengo cha  Ugavi na Ununuzi  wa hospitali hiyo Iddi Lemmah wakimsikiza CPA. Cosmas Mbogela wakati akitoa  mafunzo ya jinsi ya kutambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaji kazi wa hospitali hiyo yanayofanyika  kwa siku tatu jijini Dar es Salaam. ************************************************************************************************************************************************************************************** Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group wanahudhuria   mafunzo ya kutambua na kudhibiti vihata...

Watoto 9 wafanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio JKCI

Image
Wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel   wakizibua mshipa wa damu wa moyo wa mtoto uliokuwa umeziba,  kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalumu ya matibabu kwa watoto iliyomalizika hivi karibuni. *************************************************************************************************************************************************************************************************************** Watoto tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio kwenye kambi maalumu ya matibabu ya siku mbili iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Upasuaji huo umefanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel. Akizungumza na waandishi wa habari Dakt...

Shindano la uandishi wa Insha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari"Moyo W...

Image

Zawadi nono kutolewa kwa washindi uandishi wa Insha Mashuleni "Moyo Wangu Afya Yangu"

Image

JKCI yawagusa wananchi wa Anjouan – Wagonjwa 852 wapatiwa huduma za matibabu ya moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan Dkt. Ibrahim Salim Mari mara baada ya kumaliza kwa kambi ya matibabu ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania wakiwemo wa moyo iliyokuwa inatolewa kwa wananchi.   Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akiangalia dawa anazotumia Abdouloihid Idarouse mkazi wa kisiwa cha Ngazidja ambaye alifanyiwa upasuaji kwa njia ya tundo dogo wa kuzibua mshipa wa damu wa moyo uliokuwa umeziba katika taasisi hiyo. Idarouse alifika katika hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan ambako madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania wakiwemo wa JKCI walikuwa wanatoa huduma za matibabu kwa wananchi. Mtaalamu wa vipimo vya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gerson Mpondo akimkabidhi mkazi wa kisiwa cha  Anjouan  Soufiane Mohamed maj...

Wagonjwa 9 wenye matatizo ya mishipa mikubwa ya damu kutanuka na kupasuaji wafanyiwa upasuaji JKCI

Image
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya na Afisa Muuguzi wa Taasisi hiyo Mahawa Asenga wakimkabidhi mtaalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi (Heart Lung Machine) kutoka Shirika la Cardio Start Internation la nchini Marekani Kim Bekker zawadi wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuji wa moyo iliyokuwa ikifanyika katika Taasisi hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki. Jumla ya wagonjwa 9 wenye matatizo ya mishipa ya damu kutanuka au kuchanika wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo. Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akimkabidhi Rais wa Shirika la Cardio Star International la nchini Marekani Dkt. Miroslav Peev tuzo ya kutambua mchango wao katika kubadilisha ujuzi wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuji wa moyo iliyokuwa ikifanyika katika Taasisi hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki. Jumla ya wagonjwa 9 wenye matatizo ya mi...

JKCI – Hospitali ya Dar Group yafanya matibabu ya bila malipo kwa wakazi 251 wa Mbagala na maeneo jirani

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Masanja James akimshauri mwananchi wa Temeke mara baada ya kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyokuwa ikifanywa na Hospitali hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 251 walifanyiwa uchunguzi wa afya. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Ibrahim Amri akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ijulikanayo kama Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyokuwa ikifanywa na Hospitali hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 251 walifanyiwa uchunguzi wa afya. Baadhi ya wakazi wa Mbagala wakiwa katika foleni ya kupima shinikizo la...

Comoro yaja kujifunza huduma za afya za kibingwa nchini

Image
Waziri Mwandamizi wa Comoro Mhe. Dkt. Aboubacar Anli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipotembelea Hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan kwaajili ya kuona kambi ya matibabu inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania. Waziri Mwandamizi wa Comoro Mhe. Dkt. Aboubacar Anli akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipotembelea Hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan kwaajili ya kuona kambi ya matibabu inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa Comoro Dkt.  Mohamed Soudjay akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu na madaktari bingwa kutoka Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao chao cha kuangalia namna ambavyo nchi hizo zitaimarisha uhusiano katika sekta ya afya.   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi y...

Magonjwa ya kinywa yatajwa kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Image
Daktari wa kinywa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Aitham Mohamed akichunguza kinywa cha mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanywa na Hospitali hiyo katika viwanja vya Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Helman Nicholaus akipima mapigo ya moyo ya mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanywa na Hospitali hiyo katika viwanja vya Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Irene Ngowi akimshauri mwananchi wa Mbagala mara baada ya mwananchi huyo kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Su...

JKCI kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) kuboresha matibabu ya moyo barani Afrika

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya tathmini ya huduma za matibabu ya moyo zinavyotolewa na taasisi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika Dkt. Adamu Isah, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Malya na wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kutathimini huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo. Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Malya, Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane na wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) wa...