Comoro yaja kujifunza huduma za afya za kibingwa nchini


Waziri Mwandamizi wa Comoro Mhe. Dkt. Aboubacar Anli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipotembelea Hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan kwaajili ya kuona kambi ya matibabu inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania.

Waziri Mwandamizi wa Comoro Mhe. Dkt. Aboubacar Anli akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipotembelea Hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan kwaajili ya kuona kambi ya matibabu inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Tanzania.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa Comoro Dkt. Mohamed Soudjay akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu na madaktari bingwa kutoka Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao chao cha kuangalia namna ambavyo nchi hizo zitaimarisha uhusiano katika sekta ya afya.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mkazi wa  kisiwa cha Anjouan aliyefika katika hospitali ya Hombo kwaajili ya kupata huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa kwa wananchi wa kisiwa hicho. Kushoto ni Daktari wa taasisi hiyo Janeth Mmari.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Letara akimpima mapigo ya moyo mtoto aliyefika katika hospitali ya Hombo iliyopo kisiwa cha Anjouan kwaajili ya kupata huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na madaktari bingwa kutoka Tanzania kwa wananchi wa kisiwa hicho.

**********************************************************************************************************************************************Wataalamu wa afya kutoka Comoro wanatarajiwa kufanya ziara nchini Tanzania ili kuona huduma za matibabu ya ubingwa bobezi zinazotolewa katika hospitali zilizopo nchini na kujifunza jinsi wagonjwa kutoka nchi yao wanavyoweza kupata matibabu ya kiwango cha juu.

Ziara hiyo ni sehemu ya ushirikiano wa kitaalamu katika sekta ya afya kati ya nchi hizo mbili ikilenga kuboresha huduma za matibabu na kuimarisha ushirikiano wa afya.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa Comoro Dkt. wakati akiongea na madaktari bingwa kutoka Tanzania wanaotoa huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali katika visiwa vya Anjouan.

Dkt. Soudjay aliongeza kuwa mbali na kutembelea hospitali, wataalamu hao pia watatembelea vyuo vya afya vilivyopo Tanzania ili wanafunzi wa Comoro waweze kusoma katika mazingira rafiki ambayo ni karibu na familia zao na mila zinazofanana.

“Lengo la ziara hii ni kujenga timu za kitaalamu zinazoshirikiana kama ndugu. Wataalamu wetu wengi wakipata ujuzi, kila kisiwa cha Comoro kitakuwa na daktari bingwa hii itawasaidia  wananchi kutosafiri kutoka kisiwa kimoja kwenda kingine kutafuta huduma”,  alisema Dkt. Soudjay.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu alisema ni muhimu kwa wataalamu wa afya kutoka Tanzania na Comoro kushirikiana kwa karibu, kwani wananchi wengi wa Comoro wanapata huduma za matibabu ya kibingwa nchini Tanzania.

“Tunaomba tarehe rasmi ya wataalamu wenu kuja kututembelea Tanzania ili tuweze kujiandaa. Tunathamini sana ushirikiano uliopo baina yetu”,  alisema Mhe. Balozi Yakubu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tiba Taifa, Dkt. Peter Kisenge alisema ziara hiyo ya wataalamu wa afya kutoka Comoro itaimarisha ushirikiano wa kitaalamu kati ya nchi hizi mbili na kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wa Comoro.

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa