JKCI kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) kuboresha matibabu ya moyo barani Afrika
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa
Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah alipotembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya tathmini ya huduma za matibabu ya
moyo zinavyotolewa na taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika Dkt. Adamu Isah, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Malya na wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kutathimini huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka
Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Malya, Mkurugenzi wa Idara ya
Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane na
wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumalizika kwa ziara ya kutathimini huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na
JKCI.
Na JKCI
****************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kusaini
makubaliano
maalumu na Umoja wa Afrika (AU) kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa
wafanyakazi wa umoja huo ikiwemo kuwaleta
baadhi ya wagonjwa wa moyo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge alisema taasisi
hiyo itashiriki katika uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja
wa Afrika (AU) pindi wanapofika hapa nchini kwa mikutano.
“Ujio
wa ujumbe kutoka Umoja wa Afrika (AU) unaonesha namna Tanzania inavyotambulika
kwa ubora wa huduma za
kibingwa za matibabu ya moyo barani Afrika. Tumetembelewa na
kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali yetu chini ya uongozi wa Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan”, alisema Dkt. Kisenge.
Aliongeza
kuwa baada ya kufanya tathmini ya kina, ujumbe wa Umoja wa Afrika (AU)
uliridhishwa na ubora
wa huduma, miundombinu, na wataalamu waliopo JKCI, na hivyo kukubali kuingia makubaliano maalumu ili taasisi hiyo
iwe kituo cha kuwahudumia wafanyakazi wa Umoja wa Afrika na wananchi wa nchi
mbalimbali barani Afrika.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi
Huduma za Tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU), Dkt. Adamu Isah, alisema wametembelea JKCI ili kutathmini uwezo wake
na kujadiliana juu ya ushirikiano wa kimatibabu, na waliridhishwa na walichokiona.
“Tumevutiwa
sana kiasi kwamba wafanyakazi wetu wa Umoja wa Afrika wataweza kupata huduma
za matibabu ya moyo hapa bila kwenda Ulaya au sehemu nyingine,” alisema Dkt. Isah.
Aliongeza
kuwa hatua hii inapongeza uwekezaji mkubwa wa serikali ya Tanzania katika sekta
ya afya na inapaswa kuigwa na nchi nyingine barani Afrika, huku ikilenga
kutimiza dira ya Umoja wa Afrika ya “Afrika Tunayoitaka.”
Naye
Mkurugenzi wa Magonjwa
ya Moyo wa JKCI Dkt. Tatizo Waane alisema ziara hiyo
inalenga kuimarisha ushirikiano
kati ya Tanzania na nchi jirani.
“Ziara
hii ni sehemu ya kuunda
mtandao wa huduma za afya barani Afrika, tukishirikiana na
nchi jirani kama Zambia, Kongo, Zimbabwe, Kenya, Uganda na nyingine, katika
kutoa huduma bora za magonjwa ya moyo,” alisema Dkt. Waane.
JKCI
imeendelea kuwa kinara
wa kutoa huduma za matibabu ya moyo barani Afrika, huku ikipokea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali na
ujio wa ujumbe wa Umoja wa Afrika (AU) unatarajiwa kuongeza ushirikiano na
nafasi ya Tanzania kama kitovu cha ubora wa huduma za afya barani Afrika.



Comments
Post a Comment