JKCI – Hospitali ya Dar Group yafanya matibabu ya bila malipo kwa wakazi 251 wa Mbagala na maeneo jirani
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya
Dar Group Masanja James akimshauri mwananchi wa Temeke mara baada ya kufanya
uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyokuwa ikifanywa na Hospitali
hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mbagala Zakhem
vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 251 walifanyiwa uchunguzi
wa afya.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Ibrahim Amri akimpima kiwango cha sukari kwenye damu
mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya
ijulikanayo kama Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyokuwa
ikifanywa na Hospitali hiyo na kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya
Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 251
walifanyiwa uchunguzi wa afya.
Baadhi ya wakazi wa Mbagala wakiwa katika foleni ya kupima
shinikizo la damu wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyokuwa ikifanywa na Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group na kumalizika mwishoni mwa
wiki katika viwanja vya Mbagala Zakhem vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Jumla ya watu 251 walifanyiwa uchunguzi wa afya.
Na JKCI
*****************************************************************************************************
Watu 251 kutoka Wilaya ya Temeke kata ya Mbagala na vitongoji
vyake wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo
magonjwa ya moyo, ngiri, vidonda sugu, matatizo ya mifupa na mgongo pamoja na tiba
ya kinywa na meno.
Matibabu hayo yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Group yamefanyika katika
kambi maalumu ya siku mbili ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
tiba mkoba na kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mbagala Zakhem
vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo Daktari bingwa wa
upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Daudi Wapalila alisema asilimia
kubwa ya watu waliofanyiwa uchunguzi katika kambi hiyo walikutwa na matatizo
mbalimbali ya meno.
Dkt. Wapalila alisema baada ya kuwafanyia uchunguzi watu
waliojitokeza katika kambi hiyo watu 198 walikutwa na magonjwa mbalimbali hivyo
kupewa rufaa kufika JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya vipimo zaidi na
kuanzishiwa matibabu.
“Watu 38 waliofanyiwa
uchunguzi katika kambi hii tumewakuta na matatizo ya shinikizo la damu na
sukari, watu 18 walikuwa na shida mbalimbali za mifupa hivyo kuhitaji uchunguzi
zaidi, watu 120 walikuwa na shida mbalimbali za meno zilizohitaji uchunguzi
zaidi na watu 22 walikuwa na matatizo mbalimbali ya afya yanayohitaji
upasuaji”, alisema Dkt. Wapalila
Baadhi ya wananchi waliofanyiwa uchunguzi wa afya katika
kambi hiyo waliwashukuru wataalamu kutoka JKCI kwa kuwafikishia huduma za afya
bila malipo, kuwapa elimu kuhusu afya bora na kuwahamasisha kufanya uchunguzi
wa afya mara kwa mara.
Bakari Mkumba alisema amekuwa akisumbuliwa na tatizo la
shinikizo la juu la damu hivyo kuudhuria katika hospital binafsi kufuatilia
mwenendo wa tatizo hilo lakini baada ya kukutana na wataalamu wabobezi ataanza
kufanya kliniki zake za matibabu kwa wataalamu hao.
“Kwakweli nilikuwa siamini kuhusu kambi mbalimbali za
matibabu zinazofanywa na wataalamu wa afya kutoka hospitali na vituo vya afya
mbalimbali lakini leo baada ya kufika hapa na kukutana na wataalamu wa JKCI nimepata
elimu nzuri sana pamoja na dawa za shinikizo la damu, lakini pia nimepewa mbinu
za kufuata ili tatizo hili lisisababishe madhara mengine”, alisema Bakari .
Bakari aliomba huduma hizo ziendelee kutolewa mara kwa mara kuwafikia
wananchi ili watu wote waweze kupata elimu kama ambayo ameipata yeye kwani
itasaidia kupunguza idadi ya watu wanaopata magonjwa yasiyoambukiza.
Comments
Post a Comment