JKCI na BMH waimarisha utalii tiba, wafanya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka nchini Burundi

Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye tundu kwenye moyo kutoka nchini Burundi wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanyika katika Hospitali hiyo iliyopo jijini Dodoma.

Wataalamu wa kuhudumia wagonjwa wa dharura na wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimuhudumia mtoto kutoka nchini Burundi aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye tundu kwenye moyo kutoka nchini Burundi wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanyika katika Hospitali hiyo iliyopo jijini Dodoma.

Afisa uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Wamara akitoa taarifa ya maendeleo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka nchini Burundi iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushrikiniana na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO) mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kutoka nchini Burundi wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Mtaalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sophia Lukonge akiendesha mashine hiyo wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka nchini Burundi iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Afisa Uuguzi anayefanya kazi katika chumba cha upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mahawa Asenga akiandaa vifaa vya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka nchini Burundi wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Na JKCI

***************************************************************************************************

Watoto kutoka nchini Burundi waliokuwa na matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo na watalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) hatua inayoendelea kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba Barani Afrika.

Upasuaji huo umefanyika katika kambi maalumu yenye malengo ya kuweka ushirikiano baina ya wataalamu hao, kubadilishana ujuzi pamoja na kuonesha umahiri wa wataalamu wa Tanzania katika kutoa huduma bingwa bobezi za upasuaji wa moyo kwa watoto.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Prof. Abel Makubi alisema mafanikio ya kambi hiyo yameonesha uwezo wa wataalamu wa Kitanzania kutoa huduma za kibingwa kwa kushirikiana huku ikidhihirisha matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya afya.

Prof. Makubi alisema kambi hiyo ni mwanzo wa ushirikiano kati ya BMH na JKCI ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji wa huduma za magonjwa ya moyo kwa watanzania na watu kutoka katika mataifa mengine.

Aidha Prof. Makubi alisema kambi hiyo imeandika historia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kuwa mara ya kwanza kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka nje ya Tanzania jambo linaloonesha mafanikio ya utekelezaji wa mkakati wa tiba utalii nchini.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa Watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau alisema ushirikiano huo umeiwezesha timu za wataalamu wa upasuaji wa moyo kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo wa kutoa huduma za kibingwa.

“Tumefurahia sana kupata mwaliko kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kuungana nao kutoa huduma ya upasuaji wa moyo kwa watoto waliotoka nchini Burundi, tunaziomba na Hospitali nyingine nchini zishirikiane nasi lengo likiwa ni kuongeza ujuzi na kuokoa maisha ya watoto wanaohitaji huduma za upasuaji wa moyo”, alisema Dkt. Godwin.

Naye Mratibu wa Utalii Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita alisema mafanikio ya kambi hiyo yanaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyolenga kuifanya Tanzania  kuwa kitovu cha tiba utalii Barani Afrika.

“Serikali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inataka Tanzania kuwa kitovu cha tiba utalii Barani Afrika, leo tumejionea ushirikiano wa hospitali zetu hizi mbili zilivyoanza kutekeleza maono hayo kwa vitendo”, alisema Dkt. Asha

Akitoa neno la shukrani daktari kutoka nchini Burundi Nzitunga Octavie alisema familia za watoto waliopatiwa matibabu katika kambi hiyo wameshukuru kwa ukarimu wa watanzania kuanzia mapokezi yao hadi huduma walizopatiwa.

“Tulipofika hapa tulijisikia kama tuko nyumbani tunashukuru sana madaktari wote waliofanya upasuaji wa moyo kwa watoto wetu kwani tunaamini baada ya matibabu waliyoyapata watapona”,  alisema Dkt. Octavie

Dkt. Octavie alisema kupitia kambi hiyo ameweza kujifunza mambo mengi ya kitaalamu yanayohusu magonjwa ya moyo kwa watoto kwa kufanya kazi na wataalamu wa Tanzania katika kutoa huduma kwa watoto waliotoka nchini Burundi. 

 

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi