Kwa mara ya kwanza matibabu ya uzibuaji wa mishipa ya damu ya miguu yafanyika nchini
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 100 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka Hospitali ya BLK iliyopo nchini India Suhail Bukhari wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 100 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini. Na: JKCI *****...