JKCI mshindi wa kwanza Sabasaba katika kundi na watoa huduma za afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi ngao ya mshindi wa kwanza katika kundi la watoa huduma za afya, vifaa tiba na teknolojia ihusuyo afya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa kufungwa kwa  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba leo jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo walioshiriki kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo  katika banda la JKCI wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam baada ya kufungwa kwa maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya watu 742 walipata huduma za matibabu matibabu katika banda hilo

Na: JKCI

************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la watoa huduma za afya, vifaa tiba na teknolojia ihusuyo afya wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imetolewa leo na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  wakati akifunga maonesho hayo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza nara baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alishukuru kwa tuzo walizozipata na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kila maonesho watakayoshiriki. 

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema katika banda la Taasisi hiyo walikuwa wanatoa huduma za upimaji , ushauri, matibabu na elimu ya magonjwa ya moyo.

" Katika banda letu pia tulikuwa tunatoa elimu ya jinsi ya kumuhudumia mgonjwa wa dharura,elimu hii imewasaidia watu waliotutembelea  kufahamu jinsi gani wanaweza wakawasaidia watu wengine pindi watakapopata matatizo ya ghafla ya kiafya", alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge pia alisema walikuwa wanatangaza utalii tiba kwa washiriki kutoka nje ya nchi na kuwaeleza kuwa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo zinapatikana hapa na wanaweza kuja kutibiwa kwani mazingira yao yanafanana na ya hapa nchinu tofauti na wakienda kutibiwa katika bara la Asia na Ulaya. 

Katika maonesho hayo Taasisi hiyo pia iliibuka  mshindi wa kwanza wa jumla kati ya washiriki 3431kutoka ndani na nje ya nchi .

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024