JKCI mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya Sabasaba


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda baada ya Taasisi hiyo kuibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

*****************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo yenye washiriki 3514 kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari