JKCI yashiriki mbio za Figo Marathon

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayehudumia kliniki ya VIP Odilia Njau akimpima urefu na uzito mkazi wa Dar es Salaam aliyeshiriki katika mbio za Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimpima shinikizo la damu mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyeshiriki katika mbio za Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Irene Mbonde akimkabidhi Mkuu wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila  kipeperushi kinachoonyesha huduma zinazotolewa na JKCI  wakati wa mbio za  Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki mbio za Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Picha na: Khamis Mussa

**************************************************************************************************************************


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo