JKCI kushirikiana na Chuo Kikuu cha New York Marekani katika mafunzo na utafiti


Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman wakijadiliana namna ya kushirikiana katika masuala ya utafiti na mafunzo ya magonjwa ya moyo na kubadilishana uzoefu wa jinsi  ya kufanya tafiti hizo leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akielezea namna ambavyo idara yake imekuwa ikifanya tafiti za magonjwa ya moyo wakati wa ugeni wa wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana katika masuala ya utafiti, mafunzo na kubadilishana uzoefu katika eneo la utafiti.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman kitengo cha Afya ya Jamii Prof. Anna Bershteyn akielezea namna ambavyo chuo hicho kinafanya utafiti wa magonjwa mbalimbali ya binadamu alipofika katika  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na JKCI katika masuala ya utafiti, mafunzo na kubadilishana uzoefu katika eneo la utafiti.

Muuguzi wa wodi za wagonjwa maalumu (VIP) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Cecilia Mujungu akiwaonyesha moja ya wodi hizo wageni kutoka Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba na Taasisi ya Afya  Ifakara (IHI) walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana katika masuala ya utafiti, mafunzo na kubadilishana uzoefu katika eneo la utafiti.

Picha na JKCI

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari