Mashabiki wa Arsenal Afrika watoa msaada wa milioni 16 na kuchangia damu JKCI
Mashabiki wa Arsenal Afrika kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia na Ethiopia wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati washabiki hao walipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na kutoa damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 16 kutoka kwa Mwenyekiti wa Mashabiki wa Arsenal Tanzania (ASCTZ) Raymond Anthony wakati mashabiki wa timu hiyo kutoka nchi za Afrika walipofika JKCI leo kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na kutoa damu kwa ajili ya wanaofanyiwa upasuaji. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na mashabiki wa Arsenal Afrika wakati mashabiki hao walipofika katika Taa...