Wanawake wa JKCI chachu ya mafanikio katika kutoa huduma za matibabu ya moyo nchini
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akizungumza na wanawake wa Taasisi hiyo wakati
wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila
ifikapo machi 8.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimpatia Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt.
Peter Kisenge zawadi iliyotolewa na wanawake wa taasisi hiyo wakati wa hafla
fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo
hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
JKCI Asha Izina iliyotolewa na wanawake wa taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya
kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
*******************************************************************************************
Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepongezwa
kwa kuwa sehemu kubwa ya kuleta mafanikio katika taasisi hiyo na kuifanya
kujulikana kitaifa na kimataifa.
Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Kaimu Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina wakati wa hafla fupi ya
kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Asha alisema kutokana na huduma bora za matibabu ya moyo
zinazotolewa na JKCI kumeifanya taasisi hiyo kujulikana duniani kote hivyo
wanawake wa JKCI wawe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa maendeleo hayo hayarudi
nyuma.
Asha aliwataka wanawake wa Taasisi hiyo kuimarisha mshikamano
eneo la kazi kwa kufuata miongozo ya utendaji kazi na kuleta ubora wa huduma
kwa wagonjwa wanaowahudumia.
“Sisi kama wanawake tuwe wakwanza kusimamia miongozo
kuhakikisha kuwa mwanamke akipewa kazi ya kumhudumia mgonjwa aweze kumhudumia
kwa kiwango cha juu na kuleta motisha kwa wengine kuiga mfano kwetu”, alisema
Asha
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema maendeleo mengi yanayopatikana katika
familia wanawake wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo hayo.
“Maendeleo makubwa ya Taasisi yetu yamefanywa na wanawake,
kwani tangu taasisi hii ilivyoanzishwa idadi ya wanawake ni kubwa kuliko
wanaume hivyo tunaamini mchango mkubwa hadi taasisi yetu kifikia hapa umefanywa
na wanawake.
Aidha Dkt. Kisenge aliwashukuru wanawake wote wa JKCI kwa
kuendelea kuleta upendo baina yao na kwa wagonjwa wanaowahudumia kwani wagonjwa
wamekuwa wakifarijika kuona wanahudumiwa kwa upendo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wanawake JKCI Dkt. Angela
Muhozya amewapongeza wanawake wa JKCI kwa kuwa chachu ya maendeleo katika jamii
kwa kujitoa kila wanapohitajika kwaajili ya kuisaidia jamii.
“Wanawake wa JKCI wamekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii
yetu kila tunapowahitaji kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo meeneo
mbalimbali ya Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani”,
alisema Dkt. Angela
Dkt. Angela alisema kuwa wanawake wa JKCI wamekuwa
wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo misiba, shughuli
za furaha na kuwezeshana kiuchumi kupitia mfuko wao waliouanzisha.
Comments
Post a Comment