Wataalamu wa JKCI wapatiwa mafunzo ya kujikinga na kuwakinga wagojwa na maambukizi
Mwezeshaji wa kitaifa wa mafunzo ya kuzuia maambukizi kutoka
kwa mgonjwa kwenda kwa mtoa huduma na kutoka kwa mtoa huduma kwenda kwa mgonjwa
(IPC) ambaye pia ni Afisa Uuguzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Odillo
Byabato akiwafundisha wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) jinsi ya kujikinga na maambukizi wakati wa mafunzo hayo ya siku tatu
yaliyoanza leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jilala Luchagula akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku tatu ya namna ya kujikinga na kuwakinga wagonjwa na maambukizi (IPC) yanayofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Flora
Kasembe akielezea namna ya kujikinga na maambukizi wakati wa kutoa huduma kwa
wagonjwa wakati wa mafunzo ya siku tatu ya namna ya kujikinga na kuwakinga wagonjwa
na maambukizi (IPC) yanayofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika makundi ya kujadilina wakati wa mafunzo ya siku tatu ya namna ya kujikinga na kuwakinga wagonjwa na maambukizi (IPC) yanayofanywa na wawezeshaji wa kitaifa wa mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
******************************************************************************************
Comments
Post a Comment