Upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto mkoani Arusha
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akigawa vipeperusha vya lishe na shinikizo la juu la damu kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya waliofika kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya City Park Garden. Jumla ya watu 751 walipata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi hiyo. ******************************************************************************************************************************************************************************************************* Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 08/03/2025 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha tutatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo...