Wagonjwa 14 ambao mishipa yao ya damu ilikuwa imeziba kwa muda mrefu wafanyiwa upasuaji wa moyo
Wataalamu
wa upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na mwenzao kutoka Chuo cha shams kilichopo nchini
Misri Prof. Atef Mohamed wakimfanyia upasuaji wa kuzibua mshipa wa damu ulioziba
kwa muda mrefu (chronic occlusion) mgonjwa wakati wa kambi maalumu ya siku tano
iliyokuwa ikifanyika katika Taasisi hiyo hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa 14 ambao
mishipa yao ya damu ilikuwa imeziba kwa muda mrefu wamefanyiwa upasuaji huo.
Comments
Post a Comment