JKCI yapata tuzo mdhamini mkuu mkutano wa eGA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Philip Mpango akimpatia tuzo ya mdhamini mkuu wa mkutano wa tano wa mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Salehe Mwinchete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)
jijini Arusha.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Salehe Mwinchete akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa
washiriki wa mkutano wa tano wa mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaofanyika
katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.
Maafisa Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakifuatilia mada zilizokua zikiendelea wakati wa mkutano wa tano wa mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) unaofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Arusha (AICC) jijini Arusha.
Na: JKCI
************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepewa tuzo ya
mdhamini mkuu wa mkutano wa tano wa mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Tuzo hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
uliofanyika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.
Tuzo hiyo imetolewa kutokana na udhamini uliofanywa na
taasisi hiyo wa kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa washiriki pamoja na kutoa
huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa washiriki wote bila malipo.
Katika kutoa huduma ya upimaji taasisi hiyo imeweka mashine
za kisasa za kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ambazo zinauwezo wa kuchunguza
magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watakaofanya vipimo hivyo.
Vipimo ambavyo washiriki wa mkutano huo wanapimwa ni pamoja
na kipimo cha kuangalia wingi wa sukari katika damu, kipimo cha kuangalia
shinikizo la damu (BP), kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi
(Echocardiography – ECHO), Kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo
(Electrocardiography – ECG) pamoja na vipimo vya mbalimbali vya maabara.
Taasisi hiyo imekuwa ikifanya uchungunzi wa magonjwa ya moyo
kwa watu mbalimbali kupitia mikutano tofauti ya kitaalamu inayofanywa na
serikali pamoja na sekta binafsi lengo likiwa kufikisha huduma hizo kwa watu
wengi na kuikinga jamii na magonjwa ya moyo.
Comments
Post a Comment