Wataalamu kutoka Misri wafika JKCI kubadilishana ujuzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini Misri walipofika JKCI jana kwaajili ya kuangalia jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi pamoja na kubadilishana ujuzi.
Rais
wa Chama cha madaktari wa moyo nchini Misri Prof. Ahmed Ashraf Eissa
akiwaelezea namna Misri inavyotoa huduma za matibabu ya moyo kwa wataalamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya wataalamu hao kufika JKCI
jana kwaajili ya kuangalia jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi pamoja na
kubadilishana ujuzi.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Misri Ghada Kazamel akielezea namna ugonjwa wa shinikizo la damu unaweza kuleta madhara wakati wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Misri walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwaajili ya kuangalia jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi pamoja na kubadilishana ujuzi.
Baadhi ya wataalamu wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka nchini Misri wakisikiliza wakati wataalamu kutoka Misri walipotembelea JKCI jana kwaajili ya kuangalia jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi pamoja na kubadilishana ujuzi.
Na: JKCI
***********************************************************************************************************************
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini
Misri watembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuangalia jinsi
inavyofanya kazi na kuweka mikakati ya kushirikiana na taasisi hiyo katika
kutoa huduma za kibingwa bobezi ya matibabu ya moyo.
Madaktari hao wameongozwa na rais wa Chama cha
madaktari wa moyo kutoka nchini humo mara baada ya kusikia mafanikio makubwa
yaliyopo JKCI katika masuala ya tiba na upasuaji wa moyo.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea madaktari hao
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
alisema JKCI itashirikiana na wataalamu
hao katika kujengeana uwezo na kubadilishana ujuzi kwani Misri imekuwa katika masuala ya matibabu
hayo.
“Mbali na kushiriki na wataalamu hawa katika masuala
ya matibabu pia watashiriki katika mkutano wetu wa CardioTan 2025 utakaofanyika
Zanzibar mwezi Aprili ambapo hadi sasa wataalamu kutoka nchi zaidi ya 40 wamehaidi
kushiriki katika mkutano huo”, alisema Dkt. Kisenge
kwa upande wake rais wa Chama cha madaktari wa moyo nchini Misri
Prof. Ahmed Ashraf Eissa alisema nchi hiyo imejipanga kushirikiana na nchi za
Afrika kusambaza utaalamu wa matibabu ya
moyo.
“Tumejipanga kuiwezesha Afrika kutoa huduma bingwa bobezi za
matibabu ya moyo kwa wagonjwa ndio maana tumekuja Tanzania kupitia Samia Foundation
kuona kinachofanyika hapa na kuweza kubadilishana ujuzi”, alisema Prof. Ahmed
Prof. Ahmed alisema wataalamu wa magonjwa ya moyo wanatakiwa wanapopata
ujuzi washirikiane na wenzako ili kwa pamoja waweze kuokoa maisha ya watu
wanaohitaji huduma hizo.
“Leo tupo JKCI kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mazuri mengi inayofanya
taasisi hii, tumefika na tumeona, unapoingia tu unakutana na mandhari nzuri
pamoja na makaribisho mazuri ambayo yananifanya nijisikie kama nipo nchini
mwangu”, alisema Prof. Ahmed
Aidha Prof. Ahmed ameushukuru uongozi wa nchi ya Tanzania, uongozi
wa Wizara ya Afya na uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwakaribisha
na kuwapa nafasi ya kubadilishana ujuzi kwa pamoja.
Comments
Post a Comment