Mbeya kufikiwa na kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa ya moyo

*********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
UPIMAJI NA MATIBABU
YA MOYO MKOANI MBEYA
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) tutatoa
huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa washiriki
wa mkutano wa 109 wa Wadau wa Elimu kwa Umma na wananchi wa mkoa wa Mbeya.
Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote kwa
watoto na watu wazima tarehe 17 - 21/02/2025 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00
jioni katika viwanja vya City Park
Garden mkabala na uwanja wa mpira wa miguu Sokoine jijini Mbeya.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa
elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa
maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa
yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo
watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo na wale watakaokuwa
na matatizo yatakayohitaji matibabu ya kibingwa watapewa rufaa ya kuja kutibiwa
katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es
Salaam.
Tunawaomba
wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo
ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana kwa simu namba 0785460858 na 0735215430.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu
Letu”.
Comments
Post a Comment